KIYOA PROFILE / IFAHAMU KIYOA

P.O. Box 36109, Tungi, Kigamboni, Dar es salaam, Tanzania
KAULI MBIU:- Umoja; Upendo na Maendeleo

Friday, March 29, 2013


VIDOKEZO  VIHUSUVYO DARAJA LA KIGAMBONI



Kuanza kwa Ujenzi

 

Ujenzi wake ulizinduliwa rasmi tarehe 20 Septemba, 2012 na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Malengo Makuu ya Ujenzi wa Daraja

 

Malengo makuu ya ujenzi huu, ni kusaidia kupunguza msongamano         wa magari ambayo hupita katikati ya jiji la Dar es salaam wakati yakienda au yakitoka eneo la Kigamboni; Lengo lingine ni  kurahisisha usafiri wa watu pamoja na   mazao kwa wakazi wa kigamboni  na  pia kuongeza utalii wa pwani ya kusini mwa mkoa wa   DSM yaani eneo la Kigamboni.



Visifa Vikuu ya Daraja

-          Daraja hilo litakapokamilika litakuwa na  urefu wa mita 680;

-          Litakuwa na njia sita na magari yatalipia wakati yanavuka bahari yakitumia daraja;

-          Hakuna malipo kwa watembea kwa miguu na baiskeli;

-          Ujenzi wake utagharimu Bilioni 214.6 mpaka utakapokamilika; na

-          40% ya fedha inatolewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 60% inatolewa na     Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF.



Kuisha kwa Ujenzi

-    Ujenzi wa daraja hili umepangwa kukamilika tarehe 1 Februari, 2015.



    Pichani juu ni namna daraja la Kigamboni litakavyoonekana.






Pichani juu anayeonekana akifungua jiwe la msingi ni Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku alipokuwa akizindua ujenzi wa daraja la Kigamboni, tarehe 20 Septemba, 2012. 

 

Chanzo cha habari – www.tanroards.org

 

Ahsante mdau kwa kupenda kujua mabadiliko yanayoendea Kigamboni.