KIYOA's EVENTS/ MATUKIO MBALIMBALI YA KIYOA
KIJANA AMKA! TUMIA KIPAJI ULICHONACHO
Neno "Kipaji" kwa Kiswahili chepesi ni uwezo mtu aliozaliwa nao ambao humwezesha kufanya jambo fulani vizuri. Mfano, kipaji kinaweza kuonekena pale mtu anapokuwa amefanya vizuri katika masomo, michezo kama vile mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa mikono na mambo mengine kama vile useremala; ushonaji; umeme, mapishi, uvuvi, uogeleaji, ulinzi, n.k.
Jambo hili lililofanywa vizuri linaweza kuwa ni chanzo cha kupata umaarufu na mwishowe kumfanya mhusika kufahamika vyema katika jamii. Aidha, kuna faida nyingi ambazo mtu huzipata kutokana na kufahamika vyema katika jamii, faida hizo ni pamoja na kufahamiana na watu mbalimbali (networking) ambao ni moja ya chanzo kikuu cha mafanikio ya yeyote mwenye KIPAJI katika jamii.
KIYOA inapenda kukutia moyo ewe kijana kuwa, pamoja na changamoto nyingi zinazotukabili katika maisha yetu tunayoishi, ni vyema tukatumia vipaji tulivyonavyo ili viweze kutusaidia kutuunganisha na watu mbalimbali ambao wanaweza kuwa ni chanzo cha mafanikio katika kukabiliana na changamoto katika maisha yetu ya kila siku.
Kijana Amka!! Tumia Kipaji Ulichonacho!!!!
Pichani juu ni WanaKIYOA dada Itika Seme (mwenye koti) pamoja na dada Sara Richard wakipanga nguo mbalimbali walizozitengeneza ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Vipaji na kazi za mikono za WanaKIYOA. Maonyesho haya yalifanyika Chadibwa Beach, Kigamboni - Dar es Salaam.
Pichani chini ni baadhi ya watu waliofika kujionea maonyesho ya WanaKIYOA.
Baada ya kukamilika maonyesho na mauzo ya kazi za mikono. Zoezi lililofuata ni kujumuika na jamii katika muziki. Pichani chini WanaKIYOA wakionyesha vipaji katika kucheza muziki 'KWAITO'.
Pichani chini ni WanaKIYOA na Wanajamii wakionyesha VIPAJI katika muziki "MDUARA"
No comments:
Post a Comment