KIYOA PROFILE / IFAHAMU KIYOA

P.O. Box 36109, Tungi, Kigamboni, Dar es salaam, Tanzania
KAULI MBIU:- Umoja; Upendo na Maendeleo

Monday, February 25, 2013

KIYOA NA FEDERATION KATIKA USAFI WA MAZINGIRA TAREHE  --- 23 FEBRUARI, 2013

 

WanaKIYOA wakishirikiana na kikundi cha FEDERATION (Kikundi cha kijamii chenye makazi yake Tungi, Kigamboni), wameendelea na zoezi la usafi wa mazinngira katika eneo lililopo jirani na Shule ya Msingi Tungi, Kigamboni Dar es salaam. Zoezi hili shirikishi ni mwendelezo wa Mpango Maalum wa Usafishaji na Utunzaji wa Mazingira.

 
 
 
 

Pichani juu ni baadhi ya washiriki KIYOA na FADERATION wakati wa kuanza kwa muendelezo wa zoezi la usafi katika eneo la Tungi, Kigamboni, Dar es salaam. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tungi, Ndg. Ramadhani Kayungi (mwenye fulana nyeusi) ni mmoja wa viongozi walioshiriki zoezi hilo.

 

Pichani chini zoezi likiendelea.

 
   

 



"Hapa mpaka kieleweke!!" Pichani chini ni Ndg. Godfrey Miunguzi (Mwenyekiti Msaidizi wa KIYOA) alisikika hapa akiwahamasisha washiriki.



  

Pichani chini, Washiriki kutoka KIYOA na FEDERATION waliojitoa kwa hali na mali wakikamilisha Awamu ya Pili ya muendelezo wa Mpango Maalum wa Usafishaji na Utunzaji wa Mazingira.

 



ILANI:

NI MARUFUKU KUTUPA TAKATAKA KATIKA MAENEO YOTE
AMBAYO ZOEZI HILI LIMEKWISHA FANYIKA. 
 
WATOA HUDUMA WA "KIYOA" NA "FEDERATION" WATAPITA MAJUMBANI NA KUZOA TAKA ZILIZIZALISHWA KWA UTARATIBU ULIOKWISHATOLEWA.
 
EPUKA MADHARA YA KUTOTII SHERIA, TII SHARIA BILA SHURUTI.
ZINGATIA USAFI WA MAZINGIRA KWA AFYA YAKO NA JAMII INAYOKUZUNGUKA