UJUMBE WA LEO: "KIJANA KAZA BUTI!! USIONE VINAELEA VIMEUNDWA"
KIYOA PROFILE / IFAHAMU KIYOA
- KIGAMBONI YOUTH ASSOCIATION
- P.O. Box 36109, Tungi, Kigamboni, Dar es salaam, Tanzania
- KAULI MBIU:- Umoja; Upendo na Maendeleo
Wednesday, September 4, 2013
Thursday, May 30, 2013
KUMBUKUMBU (LEO ZAMANI)
Pichani juu ni dada Donatha Mwita akipokea cheti chake cha kuhitimu mafunzo ya
KIVUKO.
Pichani juu ni dada Ghati F. Changarawe akipokea cheti.
Pichani juu ni kaka Greyson Mwikola akipokea cheti chake. Vilevile, vijana wanaoonekana
pichani hapo chini ni baadhi ya Wanakiyoa wakionyesha vyeti walivyopokea siku hiyo.
KIYOA WAHITIMU MAFUNZO YAHUSUYO MAHUSIANO NA MAWASILIANO KATIKA JAMII (KIVUKO)- TAREHE 30 MEI, 2008.
Pichani chini ni baadhi ya WanaKIYOA wakipokea vyeti vya kuhitimu mafunzo ya mahusiano na mawasiliano (mafunzo yajulikanayo kwa jina la KIVUKO) kutoka kwa Walimu kutoka PASADA. Ilikuwa ni tarehe 30 Mei, 2008.
KIYOA inawashukuru sana PASADA kwa mafunzo haya muhimu yanayoendelea kutuunganisha pamoja vijana na kutuwezesha kuishi vyema zaidi katika jamii katika maisha yetu ya kila siku.
Pichani juu ni dada Donatha Mwita akipokea cheti chake cha kuhitimu mafunzo ya
KIVUKO.
Pichani juu ni dada Ghati F. Changarawe akipokea cheti.
Pichani juu ni kaka Greyson Mwikola akipokea cheti chake. Vilevile, vijana wanaoonekana
pichani hapo chini ni baadhi ya Wanakiyoa wakionyesha vyeti walivyopokea siku hiyo.
Friday, March 29, 2013
VIDOKEZO VIHUSUVYO DARAJA LA KIGAMBONI
Kuanza kwa Ujenzi
Ujenzi
wake ulizinduliwa rasmi tarehe 20 Septemba, 2012 na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Malengo Makuu ya Ujenzi wa Daraja
Malengo makuu ya ujenzi huu, ni kusaidia kupunguza msongamano wa magari ambayo hupita katikati ya jiji la Dar es salaam wakati yakienda au yakitoka eneo la Kigamboni; Lengo lingine ni kurahisisha usafiri wa watu pamoja na mazao kwa wakazi wa kigamboni na pia kuongeza utalii wa pwani ya kusini mwa mkoa wa DSM yaani eneo la Kigamboni.
Visifa Vikuu ya Daraja
-
Daraja
hilo litakapokamilika litakuwa na urefu
wa mita 680;
- Litakuwa na njia sita na magari yatalipia wakati yanavuka bahari yakitumia daraja;
-
Hakuna
malipo kwa watembea kwa miguu na baiskeli;
- Ujenzi wake utagharimu Bilioni 214.6 mpaka utakapokamilika; na
- 40% ya fedha inatolewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 60% inatolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF.
Kuisha kwa Ujenzi
- Ujenzi wa daraja hili umepangwa kukamilika
tarehe 1 Februari, 2015.
Pichani juu ni namna daraja la Kigamboni litakavyoonekana.
Pichani juu anayeonekana akifungua jiwe la msingi ni Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku alipokuwa akizindua ujenzi wa daraja la Kigamboni, tarehe 20 Septemba, 2012.
Chanzo cha habari – www.tanroards.org
Ahsante mdau kwa kupenda kujua mabadiliko yanayoendea Kigamboni.
Thursday, February 28, 2013
KIJANA CHACHU YA MAENDELEO
Maendeleo ni moja ya kiashiria muhimu wakati wa utekelezaji wa Dira na Dhamira ya KIYOA. Kwa mujibu wa KIYOA, "Maendeleo" ni "hali ya mtu au kundi la watu kufanikiwa kiuchumi na kijamii". Aidha, kufanikiwa kiuchumi inahusisha hali ya kujiongezea kipato kwa njia za halali wakati kufanikiwa kijamii inahusisha kuishi maisha shirikishi ambayo jamii inaweza kutatua changamoto inazozikabili kwa kupitia ushiriki wa watu wake wakati wa kutatua changamoto husika.
Kimsingi, kuna changamoto nyingi zinazowakabili watu katika jamii zao, vile vile changamoto hizi hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine. Mfano, jamii moja wakati inakabiliwa na ujinga, elimu duni, maradhi, n.k, wakati huo huo jamii nyingine inakabiliwa na majanga kama vile vita vya wenyewe kwa wenyewe, mafuriko ya maji, vimbunga, matetemeko ya ardhi, n.k.
Katika baadhi ya maeneo hapa nchini, jamii zetu zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa ni vikwazo vya maendeleo katika maeneo husika. Baadhi ya changamoto hizi ni pamoja na utumiaji wa madawa na kulevya, maradhi mbalimbali, uharibifu wa mazingira, uwezo mdogo wa kujikimu kimaisha, ufinyu wa bajeti katika kutekeleza mipango ya maendeleo, n.k.
Pamoja na jitihada zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo kutoa elimu katika kupambana na changamoto husika, mwamko mdogo kwa baadhi ya Wanajamii hususan vijana (nguvukazi ya taifa la leo) katika kujitoa kushiriki kikamilifu kusaidiana na jamii ni moja ya changamoto kubwa ndani ya jamii zilizo nyingi, changamoto hii imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa jamii husika katika kujiletea maendeleo endelevu kupitia njia ya kujitolea.
Ili tuweze kutimiza azma ya "Maendeleo Endelevu" kwa taifa letu, ni vyema vijana sasa popote tulipo tujiunge pamoja katika vikundi vya kijamii na kutumia ujuzi, taaluma na sehemu ya muda tulionao katika kisaidia juhudi za maendeleo katika jamii zetu tunazoishi.
Vijana ni vyema tukafahamu kuwa, sote kwa pamoja tuna jukumu kubwa katika kujenga jamii bora kwa kutumia sehemu ya muda wetu, ubunifu, ujuzi , taaluma na elimu tulizonazo kwa kuwa "Vijana ni Chachu ya Maendeleo katika Jamii Tunazioshi."
VIJANA TUKIAMUA!! TUNAWEZA!!
Pichani juu na chini ni baadhi ya vijana wa KIYOA wakiwashirikisha kupanda miti wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Tungi. Zoezi hilo la upandaji miti liligharimiwa na kusimamiwa na KIYOA ikiwa ni sehemu ya uboreshaji mazingira yanayoizunguka shule hiyo.
Pichani chini zoezi hilo likiendelea, wanaoonekana ni baadhi ya vijana wa KIYOA wakiwashirikisha kupanda miti walimu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Tungi.
Monday, February 25, 2013
KIYOA NA FEDERATION KATIKA USAFI WA MAZINGIRA TAREHE --- 23 FEBRUARI, 2013
WanaKIYOA wakishirikiana na kikundi cha FEDERATION (Kikundi cha kijamii chenye makazi yake Tungi, Kigamboni), wameendelea na zoezi la usafi wa mazinngira katika eneo lililopo jirani na Shule ya Msingi Tungi, Kigamboni Dar es salaam. Zoezi hili shirikishi ni mwendelezo wa Mpango Maalum wa Usafishaji na Utunzaji wa Mazingira.
Pichani juu ni baadhi ya washiriki KIYOA na FADERATION wakati wa kuanza kwa muendelezo wa zoezi la usafi katika eneo la Tungi, Kigamboni, Dar es salaam. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tungi, Ndg. Ramadhani Kayungi (mwenye fulana nyeusi) ni mmoja wa viongozi walioshiriki zoezi hilo.
Pichani chini zoezi likiendelea.
"Hapa mpaka kieleweke!!" Pichani chini ni Ndg. Godfrey Miunguzi (Mwenyekiti Msaidizi wa KIYOA) alisikika hapa akiwahamasisha washiriki.
Pichani chini, Washiriki kutoka KIYOA na FEDERATION waliojitoa kwa hali na mali wakikamilisha Awamu ya Pili ya muendelezo wa Mpango Maalum wa Usafishaji na Utunzaji wa Mazingira.
ILANI:
NI MARUFUKU KUTUPA TAKATAKA KATIKA MAENEO YOTE
AMBAYO ZOEZI HILI LIMEKWISHA FANYIKA.
WATOA HUDUMA WA "KIYOA" NA "FEDERATION" WATAPITA MAJUMBANI NA KUZOA TAKA ZILIZIZALISHWA KWA UTARATIBU ULIOKWISHATOLEWA.
EPUKA MADHARA YA KUTOTII SHERIA, TII SHARIA BILA SHURUTI.
ZINGATIA USAFI WA MAZINGIRA KWA AFYA YAKO NA JAMII INAYOKUZUNGUKA
Friday, February 22, 2013
KIJANA AMKA! TUMIA KIPAJI ULICHONACHO
Neno "Kipaji" kwa Kiswahili chepesi ni uwezo mtu aliozaliwa nao ambao humwezesha kufanya jambo fulani vizuri. Mfano, kipaji kinaweza kuonekena pale mtu anapokuwa amefanya vizuri katika masomo, michezo kama vile mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa mikono na mambo mengine kama vile useremala; ushonaji; umeme, mapishi, uvuvi, uogeleaji, ulinzi, n.k.
Jambo hili lililofanywa vizuri linaweza kuwa ni chanzo cha kupata umaarufu na mwishowe kumfanya mhusika kufahamika vyema katika jamii. Aidha, kuna faida nyingi ambazo mtu huzipata kutokana na kufahamika vyema katika jamii, faida hizo ni pamoja na kufahamiana na watu mbalimbali (networking) ambao ni moja ya chanzo kikuu cha mafanikio ya yeyote mwenye KIPAJI katika jamii.
KIYOA inapenda kukutia moyo ewe kijana kuwa, pamoja na changamoto nyingi zinazotukabili katika maisha yetu tunayoishi, ni vyema tukatumia vipaji tulivyonavyo ili viweze kutusaidia kutuunganisha na watu mbalimbali ambao wanaweza kuwa ni chanzo cha mafanikio katika kukabiliana na changamoto katika maisha yetu ya kila siku.
Kijana Amka!! Tumia Kipaji Ulichonacho!!!!
Pichani juu ni WanaKIYOA dada Itika Seme (mwenye koti) pamoja na dada Sara Richard wakipanga nguo mbalimbali walizozitengeneza ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Vipaji na kazi za mikono za WanaKIYOA. Maonyesho haya yalifanyika Chadibwa Beach, Kigamboni - Dar es Salaam.
Pichani chini ni baadhi ya watu waliofika kujionea maonyesho ya WanaKIYOA.
Baada ya kukamilika maonyesho na mauzo ya kazi za mikono. Zoezi lililofuata ni kujumuika na jamii katika muziki. Pichani chini WanaKIYOA wakionyesha vipaji katika kucheza muziki 'KWAITO'.
Pichani chini ni WanaKIYOA na Wanajamii wakionyesha VIPAJI katika muziki "MDUARA"
Thursday, February 21, 2013
ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA LILILOFANYIKA TAREHE 16 FEBRUARI, 2013
Pichani juu ni baadhi ya vijana wa KIYOA wakianza utekelezaji wa ukusanyaji na uchomaji takataka zilizoonekana katika maeneo yanayozunguka nyumba za wakazi wa Tungi Kigamboni, Dar es Salaam. Lengo kuu la zoezi hili lilikuwa ni kuwakumbusha Wananchi juu ya umihimu wa ushiriki wa pamoja katika utunzaji wa mazingira yanayotuzunguka.
Pichani juu ni dada Joanitha Joas akiendelea na ukusanyaji wa takataka zilizosambaa katika makazi ya watu.
Pichani chini ni Wadada wa KIYOA wakiendelea na zoezi la ukusanyaji na uchomaji takataka.
Pichani chini, zoezi la ukusanyaji na uchomaji takataka likiendelea katika eneo lililo katikati ya makazi ya watu na ambalo limekuwa likitumika kama dampo la takataka.
Zoezi la ukusanyaji na uchomaji takataka hatua ya kwanza lakamilika.
UJUMBE KWA WANAJAMII
NI VYEMA SOTE KWA PAMOJA TUZINGATIE MAELEKEZO NA KANUNI ZA AFYA BORA KWA KUSHIRIKI KATIKA UTUNZAJI MAZINGIRA YETU YANAYOTUZUNGUKA.
Aidha, kwa wakazi wa Tungi, Kigamboni Dar es Salaam. KIYOA inapenda kuwajulisha kuwa, utaratibu maalum wa ukusanyaji wa takataka umeandaliwa ambapo KIYOA wakishirikiana na FEDERATION watapita majumbani na kukusanya takataka zote zilizozalishwa kwenda kutupwa eneo lililoteuliwa. Wana-Tungi wote mnaombwa kutoa ushirikiano wakati wa zoezi hili.
Monday, January 28, 2013
"Umoja; Upendo na Mshikamano ndiyo nguvu yetu".
Pichani juu baadhi ya WanaKIYOA (kuanzia kulia) ni Ndg. Godfrey Miunguzi; Ndg. Shuma Mafuwe; Ndg. Greyson Mwikola; Ndg. Gerald Msuya; Ndg. Jimmy Mayunga muda mfupi kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano Mkuu wa KIYOA
Pichani chini ni baadhi ya WanaKIYOA na maeneo ya ushiriki wao katika KIYOA
Dada Itika Seme - MwanaKIYOA (Uhamasishaji)
Dada Ghat Francis - MwanaKIYOA (Fedha na Utawala)
Dada Victoria Zakayo - MwanaKIYOA ( Shughuli za Kijamii)
Kaka Godfrey Miunguzi - MwanaKIYOA (Utawala; Maadili na Miradi)
MATUKIO KATIKA PICHA MKUTANO MKUU WA KIYOA ULIOFANYIKA BARAKUDA BEACH TAREHE 26 JANUARI 2013
KUMBUKUMBU ZA MUTANO MKUU WA KIYOA
Wajumbe wakipata chakula cha mchana kabla ya kuingia awamu ya pili ya kumalizia Mkutano Mkuu wa KIYOA.
Pichani juu ni wajumbe wakimalizia kupata chakula cha mchana.
UCHAGUZI WA UONGOZI MPYA WA KIYOA KWA MWAKA 2013
Pichani chini ni Ndg. Gerald Msuya (kushoto) ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kusimamia uchaguzi wa viongozi wapya wa KIYOA. Kulia kwake ni msaidizi wake dada Judy Isomba akimsaidia kuhesabu kura.
Katika uchaguzi huo Ndg. Humphrey Msulwa alichaguliwa kuwa Mwenyekiti; Ndg. Godfrey Minguzi amekuwa Mwenyekiti Msaidizi; Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Ndg. Shuma Mafuwe; Ndg. Jimmy Mayunga amekuwa Katibu Msaidizi. Mwisho, nafasi ya Mhasibu (Mweka Hazina) imechukuliwa na Ndg. Ghati Francis Changarawe.
MKUTANO MKUU WA KIYOA WA MWAKA 2012 WAMALIZIKA
Pichani juu ni baadhi ya WanaKIYOA wakitawanyika baada ya majadiliano ya zaidi ya masaa matano yaliyowawezeha kupata maazimio ya msingi katika utekelezaji wa kazi za KIYOA.
MATUKIO KATIKA PICHA
YA MKUTANO MKUU WA KIYOA ULIOFANYIKA BARAKUDA BEACH TAREHE 26 JANUARI 2013
WANAKIYOA WAKISUBIRI KUANZA MKUTANO
Subscribe to:
Comments (Atom)